Sinaubi

Sinaubi

SwahiliEbook
Kidato, Mbwana
Mkuki na Nyota Publishers
EAN: 9789987085163
Available online
€30.40
Common price €33.77
Discount 10%
pc

Detailed information

Hii ni Riwaya ya kwanza ya Mbwana Kidato ambayo inatokana na tukio la kweli alilolisoma alipokuwa akipitia majarida mbali mbali ya Tanzania kwenye mtandao. Kwenye kurasa za mbele, alikutana na habari ya kuhuzunisha. Ilikuwa ni habari ya msichana mwenye ulemavu wa ngozi aliyekatwa viungo vya mwili wake. Hii ni kazi ya mwandishi, kazi ya kufikirika, yenye kuelimisha, kuakisi maisha yetu na kutuuliza maswali juu ya utu wetu. Je miongoni mwetu kuna wengine wana utu wenye thamani zaidi ya utu wa wengine? Kama kuna kipimo cha utu, huo utu unapimwa na kipimo cha aina gani? Je kipimo hicho ni maumbile yetu au ni tabia zetu? ama ni vitu vinavyo tuzunguka? Muandishi anajaribu kuuliza haya maswali, kupitia muhusika mkuu wa riwaya hii ambaye ni 'SINAUBI'. Mbwana Kidato ni mtengenezaji wa vipindi vya runinga na filamu. Amepata elimu yake nchini Uingereza kwenye nyanja za uandaaji, utengenezaji, uandishi na uhariri wa picha za vipindi vya filamu na runinga. Ameshawahi kufanya kazi na Shirika la Utangazaji la Tanzania, kama mtayarishaji wa vipindi. Siyo mara yake ya kwanza kuandika, (film scripts) lakini kazi yake imekuwa ikilenga zaidi hadhara ya upande wa runinga. Safari hii ameandika riwaya/tamthilia kwa hadhara yote, yaani hadhara ya wasomaji vitabu na hadhara ya waangaliaji runinga na filamu.
EAN 9789987085163
ISBN 9987085164
Binding Ebook
Publisher Mkuki na Nyota Publishers
Publication date November 11, 2024
Language Swahili
Country Uruguay
Authors Kidato, Mbwana